SHEREHE
YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU
7/6/2015
Somo I: Kut 24:3-8
Zab: 116: 12-13, 15-18
Somo II: Ebr 9: 11-15
Injili: Mk 14: 12-16,
22-26
Nukuu:
"Musa
akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu
kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda,” Kut 24:3
“Musa
akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano
alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote,” Kut 24:8
“Lakini
Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema
iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya
ulimwengu huu, wala si kwa damu
ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika
Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele,” Ebr 9:11-12
“Basi
si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake
kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo
mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?” Ebr
9:14
“Na
kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa
kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee
ahadi ya urithi wa milele,” Ebr 9:15
“Twaeni; huu ndio mwili wangu,” Mk 14:22b
“Hii ndiyo damu yangu
ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi,” Mk 14:24
“Amin,
nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile
nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu,” Mk 14:25
TAFAKARI:
“Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu!”
Wapendwa wana wa Mungu, leo Mama Kanisa
anaadhimisha sherehe ya Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mbili
kati sikukuu kubwa za Bwana wakati wa kipindi cha kawaida cha Mwaka wa Kanisa
ni: Sherehe ya Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu yetu Kristo na Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Jumapili hii katika mzunguko wa kiliturujia wa mwaka “B” wa Kanisa, Mama Kanisa
anatupatia simulizi hili kutoka Mwinjili Marko.
Mungu kwa nyakati
mbalimbali alifanya maagano na watu wake kwa malengo mbalimbali yakilenga
ushirika wake na viumbe vyake, katika safari nzima ya kuvikomboa, na hasa
mwanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi. Agano hili lilifanya kuaminiana na
kutekeleza maagizo yake kwa pande zote mbili.
"Musa akaenda akawaambia watu maneno yote
ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema,
Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda,” Kut 24:3. Mungu haikumpasa
kujisainisha katika agano kwa sababu yeye mwenyewe ni UAMINIFU, na kwamwe
katika Ukuu wake hawezi kwenye kinyume chake mwenyewe.
Maagano haya kama
ishara ikiwa ni kielelezo kwa upande wa binadamu iliendana na uteketezaji wa
viumbe vingi visivyo na doa. Damu ya viumbe hili vilihesabika maka ndiyo muhuri na kusahilisha
muungano huu wa kiagano. “Musa akaitwaa ile
damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana
pamoja nanyi katika maneno haya yote,” Kut 24:8. Hivi ni hatua za awali katika
safari nzima ya mwokovu wetu. Je, kwa nini Mungu hakulifanya jambo hili mara
moja tu na watu wake wakamwelewa? Bila shaka tendo na safari hii ya wokovu wa
Mwanadamu umepita katika hatua mbalimbali kwa lengo la kumfanya mwanadamu huyu
atambue uzuri na umaana wa thamani ya wokovu wake, na uwepo wa Mungu katika
maisha yake.
Wapendwa wana wa Mungu,
Yesu Kristo ndiye anayebadili kabisa mwelekeo na mtazamo wa sadaka hizi za
kuteketezwa. “Lakini Kristo akiisha kuja,
aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na
kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama,
bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha
kupata ukombozi wa milele,” Ebr 9:11-12. Kristo ndiye ukamilifu wa sadaka zote
zile zitolewazo. Sababu kubwa ni Mungu amependezwa na Kristo, “huyu ni Mwanangu, Mpendwa wangu,
ninayependezwa naye; msikieni yeye.” Mt 17:5. Tendo hili la utambulisha wa
Kristo kile alicho lilitanguliwa na tendo la kumwilishwa kwake. Huu ndio mpango
wa Mungu wakati ulipotimia. Hivyo, “Basi si
zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake
kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo
mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?” Ebr
9:14. Ndugu yangu unayemwamini Kristo elewa umekombolewa kwa damu yenye gharama
kubwa. Ukristo wako ni wathamani sana. Hakuna sababu ya kujiona mnyonge hata
kidogo. “Na kwa sababu hii ni mjumbe
wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa
chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele,”
Ebr 9:15
Hivyo wapendwa wana wa Mungu, leo
tunaposherehekea sherehe hii, na zaidi tunapozama katika simulizi hili la
kusimikwa rasmi kwa sherehe hii “Kitaasisi,” tendo hili latupasa kugusa ndani
kabisa ya mioyo yetu, na haizi kabisa moyo wa kuhani. Ni kuhani wa Daraja
Takatifu ambaye hulifanya jambo hili na
kuwa halisi katika nafsi ya Yesu Kristo,
zawadi ambayo hatuwezi kuielewa kwa mwono huo halisi Mbinguni. Ingawa ni ukweli
usiotia shaka kwamba tunasheherekea ukuhani wetu siku ile ya upadrisho wetu na
siku ya Alhamisi Kuu, je, haipaswi siku hii ya Sherehe ya Mwili na Damu ya
Bwana wetu Yesu Kristo, kuwa ya pekee kwa useja wetu wa Kiroho?
Injili ya leo tunakutana na maneno mazito sana, “Twaeni; huu ndio mwili wangu,”
Mk 14:22b. "wainjilisti nyingine huongeza," unaotolewa kwa ajili
yenu.” Wapendwa wana wa Mungu, siyo tu
kwamba ni Mwili wa Yesu unaotolewa, bali miili yetu pia. Nina hakika
nyote kwa asili mmegundua hatusemi "twaeni mle wote huu ni mwili wa Yesu
uliotolewa kwa anjili yenu." Ingawa ni kweli mwili wa Yesu-ukweli halisi wa uwepo wake, ambayo sisi
tunasherehekea leo vizuri na kwa maandamano, lakini pia ni miili yetu
iliyopondeka, miili ya dhambi iliyotolewa
sadaka kama kuhani / muathirika kwa ajili ya wokovu wa binadamu. Padre
kujikatalia mke na watoto, si kwa sababu wao ni wabaya (mke na watoto), bali
kwa sababu ni jambo jema sana kwa uwepo wao
la kutufanya sisi "Matowashi ajili ya Ufalme wa Mbinguni." Mt
19:12c
Ndugu yangu uzuri wa useja halisi kwa ajili
ya Ufalme wa mbinguni kama sehemu ya ufundishaji wa teología/tauhidi ya Mwili,
Baba Mtakatifu Yohane wa Pili ananukuu
Injili ya Mtakatifu Mathayo 19:21 na anafafanua juu ya zawadi ya useja ya
kuhani kwa kutoka kwa Mungu na kutoka kwa Kuhani kwa ajili ya Kanisa. Anaeleza
kwamba sisi-Makuhani tu uhuru tujongea uzuri wa ndoa kidunia na mahusiano ya
kimapenzi kama ishara ya hali ile ambayo wanaume na wanawake “wasivyoolewa au kujitoa katika ndoa.” Sisi
"Tunapita juu-“Passover"- Sakramenti Takatifu ya ndoa kwa
kutarajia/kuakisi " harusi ya Mwanakondoo." Sisi waseja ni ndoa ya
kweli - ndoa ya ushirika wa Kristo na Kanisa lake. Tumepewa zawadi kubwa ya
"upweke asili," ambayo kabla ya "umoja asili" katika shamba
la Edeni, lakini, kwa wakati na mara nyingi,
maumivu ya upweke asili;
hujisikia upweke au mzigo. Mtazamo nyacha ni kwamba maumivu ni zawadi –
mioyo yetu inahitaji kutakaswa na kuonekana hivyo na kuishi ukweli huo kwa
furaha na uhuru.
Kama ilivyo mioyo mingi inayohitaji
kutakaswa na wasiwasi, wengi wanahitaji
kusafishwa ya wasiwasi, shaka ya kuona
uwepo wa Yesu halisi katika Ekaristi Takatifu.
Huu ni wakati ambao hatutakiwi kurudi katika dhambi au kujionea huruma,
lakini kwenye maneno ya kuwekwa fumbo
hili- “Twaeni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu.” Tunaweza kuliomba hili
kwa Baba, kwa Kanisa, sisi wenyewe, kwa
ukuhani, ambayo inahitaji utakaso wa
“kikafara/kutolewa sadaka” na maombezi
kwetu sisi makuhani, ikiwa ni pamoja na walei. Je, umeshajitoa sadaka,
kufunga, kuomba na kupewa sadaka kwa ajili ya ndugu wanaojitahidi siku za hivi
karibuni au wewe mwenyewe?
Kanisa ni Bibi harusi
wetu, mzuri na bila hitilafu kwa upande
mmoja; dhambi, iliyoonekana na uliyopondeka kwa upande mwingine. Ni zawadi ya
ajabu kwetu. Hivyo ndugu zangu, kwa Bibi harusi huyu imeachwa kuona michubuko
yake, lakini hutaweza kuuona uzuri wake na heshima yake. Je, Bibi harusu huyu
ni mwili wa Kristo au siyo? Bibi harusi
huyu dhahiri ni mwili wa Kristo. Anahitaji upendo wetu, uponyaji wetu, kumbatio
letu, ulinzi wetu, heshima yetu, sadaka yetu na anahitaji ukuhani wetu na
kitolewacho sadaka. Kanisa halihitaji mara kwa mara kulalamika na kusengenya.
Kanisa linahitaji unyenyekevu wetu na umaskini wetu kama Kristo alivyojitoa
mwenyewe kwa ajili yake.
Kwa upande wetu kama ndugu katika kanisa
tunapoadhimisha Mbingu ile ni kweli, na Yesu amefufuka, na useja wetu ni
ishara huo. Jinsi tunavyoadhimisha sadaka Takatifu ya Misa
lazima kutafakari utashi wetu wa umoja
huu wa (upendo) kiuchumba kati ya Kristo na Kanisa lake. Sakramenti lazima
iadhimishwe kwa upendo mkubwa na heshima, na si kwa haraka-“kwa kulipualipua
au kiroboti roboti.” Kama mume
ajitoavyo sadaka kwa mke wake bila kujibakiza, mkewe haipaswi
kuharakisha au kuchukulia jambo hili kwa wepesi tu. Lipi lililo la muhimu zaidi
kwetu –Masakaramenti ya Mama Kanisa Takatifu au wajibu wa kiutawala ambao
lazima tuufanye? Useja ukiliishwi vizuri, unachukua mabadiliko ya Kimungu, siyo
tu malezi ya binadamu. Ni lazima kuwa na uwezo wa kuishi jambo hili kwa uhuru
na hivyo kuchukua uponyaji na ukombozi kutoka utumwa wetu wa dhambi. Uwezo wa
jambo hili kama dawa, Kristo ametupa kwa
njia ya sala/maombi na kufunga. Vikwazo
kwa mabadiliko na kuishi maisha halisi ya useja ni: dhambi isiyosemwa/kuungamwa,
majeraha yasiyoponywa na makosa
yasiyosamehewa tuyapokeayo kutoka kwa wengine na sisi wenyewe.
Tunajiheshimisha; na kuona hakuna haja ya kuwa na huruma kwetu wenyewe na
kujiweka wenyewe kila siku mbele ya uponyaji wa uwepo wa Bwana wetu wa
Ekaristi. Tendo hili haliwezi kuleta mabadiliko ndani mwetu kwa sababu bado
hatujajisalimisha sawasawa.
Mwili na Damu Takakatifu ya
Yesu ni uwepo alisi na inapaswa kuadhimishwa hivyo, lakini pia, sisi makuhani,
licha ya kuonekana katika hali ya kupondeka, tunayo haja ya kusherehekea uzuri halisi wa ukuhani,
kwa sababu ni sisi, na kwa kushuka kwake Roho Mtakatifu, anayefanya uwepo alisi wa
Yesu katika Ekaristi Tatakatifu -Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa
ajili yenu!
Bibi Betina kila mara alipohudhuria Misa
Takatifu hakuacha kukominika kwa kutumia mikono yake. Tendo hili kwake lilikuwa
la kawaida sana na hakuwa na subirá ya kuangalia mikono yake baada ya kuula
mwili wa Kristo. Ila alikuwa na furaha sana siku moja akikutana na Yesu huko
Mbinguni.
Miaka ilienda na mwisho wa uhai wake hapa
duniani ulifikia kikomo. Basi alibahatika kumwona Yesu, lakini mara hii kama
Hakimu mwenye haki. Mbele ya kiti hiki cha Hukumu, Yesu alimwuliza swali, Je,
ulishawahi kukutana nami hata mara moja katika maisha yako? “Nimekutana nawe
kila siku ya adhimisho la Misa Takatifu katika maumbo ya mkate na divai,” Bibi
Betina alijibu kwa furaha.
Kwa masikitiko Yesu alimjibu, “Ni kweli ulikutana nami katika maumbo hayo, ila
hukuweza kukaa nami kwani ulinipokea na kunibwaga chini.” “Mbona sikuelewi
Bwana wangu?” Bibi Betina alijibu kwa unyonge. “Ulinipokea katika mikono yako,
na baada ya kula kile ulichokionekana kwa macho yako, hukuwa na muda wa
kutazama mabakizo yangu. Ulijifuta mikono yako kwa mavazi ya nguo zako na mara
nilidondoka chini na kukanyagwa na watu. Hivyo hukuwa na haja nami. Nibaki
Kanisani.” Yesu alimjibu kwa utulivu. Hivyo huna makao yako huku. Nafasi zenu
zipo upande ule wa pili kwenye barabara ile pana.
Hapa ndipo kwenye kilio na kusaga meno!
Tumsifu Yesu Kristo.
No hay comentarios:
Publicar un comentario