JUMATATU
WIKI YA 11 YA MWAKA-B
15/6/2015
Somo:
2Kor 6:1-10
Zab:
97:1, 2-3ab, 3cd-4
Injili:
Mt 5:38-42
Nukuu:
“Tusiwe
kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe,”
2Kor 6:3
“Kama
wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha
wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote,” 2Kor 6:10
“Lakini
mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume,
mgeuzie na la pili,” Mt 5:39
“Akuombaye,
mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo,” Mt 5:42
TAFAKARI:
“Tuongozane katika Utakatifu, na maisha yetu yawe ushuhuda wa kweli kama
wafuasi wa Kristo.”
Wapendwa wana wa Mungu,
licha ya kwamba kila mmoja wetu ameitwa kuishi mtindo wa wamaisha kadiri ya
wito wake, “tuongozane katika utakatifu,
na maisha yetu yawe ushududa wa kweli kama wafuasi wa Kristo.” Kila mmoja
kadiri ya wito wake unaoendana na mtindo wa maisha aliouchagua, anaitwa kuwa
mtakatifu. Kwa sababu hii, mchango wangu kwa jamiii inayonizunguka nikuwafanya
watu wajue thamani ya maisha yao, na waishi katika utimilifu huo wakitafuta
zaidi ya kile walichokipata, utakatifu wao.
Hivyo, hatupaswi kuwa
sababu ya mkwamo wa wowote juu ya
kumjiua, kumpenda, kumtumikia Mungu. Tusiwe sababu ya kuwakwaza watu
katika imani yao. Tulipewa dhamana ya uongozi kadiri ya madaraja yetu,
tumtambulishe Kristo kwa watu kama alivyo. “Tusiwe
kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe,”
2Kor 6:3. Wapo ambao kati yetu kila wanapokuwa badala ya kuimarisha imani
wanakuwa chanzo cha mtafaruku wa Imani hiyo na kuwafanya waamini kuwa waasi wa
Imani yao.
Kuishi maisha ya
Kiimani kama yalivyo ni sadaka kubwa sana. Zipo nyakati ambazo utajaribiwa ili
uonyeshe ukweli wa kila unachokiishi na unachokishuhudia kwa wengine. Hakuna
sababu ya kujipamba kwa kile ambacho si chako na hukiishi. Mtazamo wetu katika
uhasilia wa vitu ni huu: “Kama wenye
huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi;
kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote,” 2Kor 6:10. Matatizo katika
maisha yetu hayapaswi kuwa ukuta wa kutufanya tusiweze kuona mbali. Matatizo ya
hapa duniani yatuweke baribu na Mungu ili tuweze kutafakari vizuri neno lake.
Maisha yetu leo
yametawaliwa na dhana ya ushindani na linganishi. Wapo kati yetu kila kukicha
ni kutafuta zaidi ya kile alichokuwa nacho hata kama kinamtosha. Mtindo huu wa
maisha hautoa taswira ya kushindwa au kuthamini
mchango wa wengine. Mwenye tabia hii
hujiamini kulikopindukia. Hivyo hapa inaitajika busara ya hali ya juu.
Hivyo twapaswa kutoandamana na ya ulimwengu kama yanavyotutaka kila siku ya
maisha yetu. Tuwe wepesi wa kusikiliza, na kusema pale tu pale inapotubidi
kufanya hivyo.
Maadili ya Kikristo yanatuwasa mara zote
kutokulipiza kisasa au kuishi katika visasi. Hivyo, “Msishindane
na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili,” Mt
5:39. Hapa tunafundishwa unyenyekevu katika kutenda. Ni katika utendaji huu
kunatufanya kuwa karibu na kila mmoja wetu tutakaye kutana naye. Wote ni ndugu
na jamaa zetu. Hivyo,
“Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo,”
Kutokujali kama Mkristo ni kujivua vazi lako
la Kikristo na kuvaa upangani au ushetani.
Tumsifu Yesu Kristo!
UTAKATIFU NDIYO CHEO
CHETU, EE YESU TUONGOZANE KATIKA
UTUAKATIFU KILA SIKU. AMINA
No hay comentarios:
Publicar un comentario