miércoles, 17 de junio de 2015

TAFAKARI: ALHAMISI WIKI YA 11 YA MWAKA-B

ALHAMISI WIKI YA 11 YA MWAKA-B
18/6/2015
Somo: 2Kor 11:1-11
Zab: 110:1-2, 3-4, 7-8
Injili: Mt 6:7-15
Nukuu:
Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu,” 2Kor 11:5

Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda,” 2Kor 11:9

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi,” Mt 6:7

Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu,” Mt 6:12

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu,” Mt 6:14-15

TAFAKARI: Kujenge utu na heshima katika kazi; Sala na kusamehe katika mahusiano yetu na Mungu.”

Wapendwa wana wa Mungu, ukitazama historia nzima ya wokovu wetu utagundua jambo hili; tumeumbwa kwa kazi, Tumekombolewa kwa kazi, na tunaishi kwa kazi. Hivyo kazi ni sehemu ya kuwepo kwetu, kuishi kwetu, na kuendeleza uumbaji wa pili wa Mungu kama viumbe vyake shirikishi (Co-creators of God). Kwa mantiki hii kazi hutujengea utu na heshima tuifanyapo kwa uaminifu. Kazi utupatia kipato chetu alali tuifanyapo kwa uaminifu. Mtume Paulo anasema hivi, kutokana na kazi yake na uaminifu wake katika kazi hiyo, “sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu,” 2Kor 11:5. Kazi inampatia Mtume Paulo heshima na nguvu ya kimaadili.

Kazi humjengea mtu utu wake. Maisha tegemezi kwa aliye na afya njema, na nguvu za kutosha hata kama husengenywi, ni fedheha kubwa katika familia na jamii. Leo kumezuka mtindo wa Wanawake kuwaadhibu wanaume zao wazembe kwenye family zao hasa nchini Kenya. Adhabu hii imepelekea hata kuwaondolea viungo vyao vya uzazi. Leo mwanaume yule alionekana kichwa cha familia na samba wa familia yake, amejeuka kuwa goigoi. Haki wanaume wanaishi katika fedheha kubwa sana leo.

Hata kama kazi humjengea mtu utu wake, utu aliokuwa nao mtu huwezi kuondelewa kwa vile hafanyi kazi katika maana ya kwamba hakuna kazi ya kufanya. Kuna ukweli pia wapo wanaume na wanawake ambao hawapendi kazi. Ni wavivu wa kupindukia na uwepo wao uzidisha mduara wa umasikini katika familia na jamii inyomzunguka.

Watu wa mtindo huu lazima waonywe na kuhimizwa kufanya kazi. Mtume Paulo anasema, Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda,” 2Kor 11:9. Vijana wenzangu tuachane na “ugali wa shikamoo.” Ugali wa shikamoo ni kwamba una miaka zaidi ya 30 bado upo nyumbani huna kazi yoyote na hupenda kujishughulisha. Kila kukicha lazima umsalimie Mzee nyumbani ili mchana upate ugali, ili hali ilikuwa ni nafasi yako kuanza kuchangia uwepo wa ugali huo kwa wazazi wako au familia yako.

Pamoja na kazi kutujengea utu na heshima, tunaitaji maisha ya sala na msamaha kujenga mahusiano mazuri kati yetu na Mungu. Binadamu siyo kisiwa. Ni katika sala Mungu huzidi kufungua neema zake na baraka kwa yale tunayofanya kwa uaminifu kila siku. Pia ni katika kusamehe kunajazwa pia neema na baraka, na hata kusamehewa mapungufu yetu mbele ya Mungu. Sala anayo tufundisha Bwana wetu Yesu Kristo leo, ili kuyapata yote tuyaombayo kuna sharti moja lazima tulitimize, yaani makosa yetu husamehewa na Mungu kwa mizania ile ile tuitumiayo kuwasamehe wale waliotukosea.Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu,” Mt 6:12. Pili kuzama katika sala ni kusali katika utulivu. Hivyo Yesu anasema,Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi,” Mt 6:7. Je, sala hii ya Baba Yetu ina maana yoyote kwa wabebao mzigo wa visasa, chuki, na kutokusamehe?

Wapendwa katika Kristo, mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu,” Mt 6:14-15. Je kunafaidha gani kutembea na gunia hili la chuki, visasi, na kutokusamehe? Kwa nini hutaki kumsamehe huyo uliyembeba muda wote katika kichwa na moyo wako? Kwa nini hutaki kujiweka huru? Yawezekana aliyekutenda hilo usilotaka kusamehe hana habari na ugomvi wako nawe. Yeye yupo huru ila wewe bado upo maabusu bila kujua tarehe rasmi ya kusikiliza kesi yako.

Tumsifu Yesu Kristo!

TUMEUMBWA KWA KAZI, TUMEKOMBOLEWA KWA KAZI, NA TUNAISHI KWA KAZI.


No hay comentarios:

Publicar un comentario