jueves, 22 de diciembre de 2016

TAFAKARI: DECEMBA 24, WIKI YA 4 YA MAJILIO


DECEMBA 24, WIKI YA 4 YA MAJILIO

Somo: 2Sam 7:1-5, 8b-11, 14a, 16

Zab: 89:2-3, 4-5, 27, 29

Injili: Lk 1: 67-79

Nukuu:

“Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake? Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli,” 2Sam 7:5b

“nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani,” 2Sam 7:9

 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa,” Lk 1:68

Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia,” Lk 1.71

“Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,” Lk 1:74

“Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao,” Lk 1:76

“Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani,” Lk 1:79

TAFAKARI: “Kwa kuwa amewajia watu wako, na kuwakomboa.”

Wapendwa wana wa Mungu, kinachogusiwa katika somo letu la kwanza ni yale yaliyojiri katika nyakati za mwisho za Mfalme Daudi. Ufalme wake katika miaka yake hiyo ya mwisho ulikuwa imara na watu wake walifurahia amani ya kweli. Licha ya kwamba Mfalme Daudi alimiliki jumba zuri la kifalme alikosa nyumba ya heshima kwa ajili ya kuhifadhi sanduku la agano. Nabii Nathani anamkumbusha wajibu huo muhimu wa kufanya Mfalme.

Ujumbe wa Mungu kwa Mfalme Daudi ulisema hivi, “Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake? Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli,” 2Sam 7:5b. Ujumbe huu ulimtaka Mfalme Daudi kwa ukarimu wake uwe kigezo pia cha kuona ukarimu wa Mungu. Hivyo yampasa kufanya kitu kuhusu Sanduku lile la Agano lihifadhiwe mahali pazuri zaidi. Yatupasa kuwa wakarimu zaidi kwani kwa uwepo wetu duniani hapa ni ukarimu mkubwa sana wa Mungu.

Hivyo agano lililowekwa katika mlima sinai linawekwa katika uhalisia wake. Ujumbe huu pia unahusisha yaliyosemwa na Nabii Isaya, 9:6, kwa kuzaliwa mtoto na mfalme wa Amani, na uokoaji wake, Lk 1:32, 69, kwa kupewa kiti cha Baba yake Daudi na kuwa pembe ya wokovu. Hivyo Masiha atakuwa mtoto wa Daudi, na ufalme wake utakuwa ufalme wa milele. Undani wa habari hii tunakutana nao katika utenzi wa Zakaria uliobeba Injili yetu ya leo.  

Wapendwa wana wa Mungu, “Zakaria akajazwa Roho Mtakatifu, na kutoa unabii.” Maneno haya yanaonekana kutumika katika maana yake pana ya uhihisho utamkwao katika hali ya kupongeza na sifa juu ya makuu mtu aliyotendewa na yenye kustaajabia. Mfano wa hali hii tunakutana nayo (katika kitabu cha kwanza cha Samueli 19:20; na waraka kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho 14: 24-25). Utenzi au wimbo  huu wa Zakaria unaonekana kama taarifa iliyoandikwa, pengine, na Zakaria mwenyewe, kwa kusifu mara maada ya kurudishiwa uwezo wake wa kuongea tena.

Maneno katika utenzi huu yawezekana ni tafakari aliyokuwa nayo kipindi kizima cha yeye kutokuongea. Ni tafakari iliyozama ndani kabisa katika matendo Makuu ya Mungu kwake na kwa Taifa zima la Israeli. Utenzi wenyewe wa Zakaria ndio uliobeba Injili yetu ya leo. Ni vyema tukatafakari kwa undani juu ya utenzi huu, Lk 1:67-80.

Zakaria alikuwa bubu alipoacha kuamini ujumbe ule wa Malaika juu ya uwezo wa Mke wake kuzaa. Ububu wa Zakari ni matokeo ya kutokuamini makuu ya Mungu. Midomo yake ikafunguka wakati alipoamini. Zakaria ni wa mwisho kati ya Manabii wa Agano la Kale, ingawa Yohane yeye alikuja kukaribisha Angano Jipya {Mathayo 11: 9 - Mathayo 11:11}. Kwa maana hiyo, Zakaria alikuwa nabii wa mwisho wa mpango wa Agano la Kale, kabla ya kuja kwa mtoto wake kwa kuhusisha Agano la Kale na Agano Jipya], aliyekuwa karibu sana na kuja kwake Masiha. Wimbo wa Zakaria unachukua Mwangwi wa zamani zote, na kuviyeyusha ndani ya mwanga mpya wa matumaini.

Utenzi au wimbo huu wa Zakaria tunaweza kuugawa katika sehemu kuu tatu: sehemu ya kwanza ni {Luka 1:68 - Luke 1:75}, habari tukutanayo hapa ni kuhusu adhimisho la  kuja kwa Masihi, kwa namna ya pekee katika kuikomboa Israeli kutoka maadui zake. Sehemu ya  pili ni {Luka 1:76 Luka 1:77}, habari za sehemu hii zipo katika lugha ya picha zaidi juu ya sintofahamu ya huyu ‘mtoto’ Yohane. Na sehemu ya tatu na ya mwisho, {Luke 1:78 - Luke 1:79}, inaturudisha katika wazo msingi kuhusu Masiha, lakini sasa linagusa juu ya suala la kuja kwake kama Mwanga kwa wote wanaokaa katika giza.

Kama tunakumbuka kwamba miaka mia nne ya sintofahamu juu ya Taifa hili la Israeli, kwa sehemu kubwa Waisraeli walikuwa chini ya mateso na dola ya kigeni, ilikuwa imepita tangu mwisho wa Manabii.  Hivyo kwa  wakati huo wote macho yao mchana na usiku yalionekana  kunyong'onyea kwa kumsubiri Masiha aliyeahidiwa. Katika mazingira haya na ishara zilizokuwa zinaambatana na tukio hili, ni wazi sasa tunaweza kuona yaliyokuwa yameujaza moyo wa Zakaria. Ni wazi kwa ishara hizo saa imewadia, na kwamba mtoto hivi karibuni kuzaliwa atatimiza ahadi ya Mungu na kukidhi matumaini yake yaliyoanza kutoweka.

Si ajabu kwamba maneno yake ya kwanza ni mpasuko wa  baraka za 'Mungu kwa wa Israeli.' “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa,” Lk 1:68. Haya ni matamshi yaliyo bora na ya hali ya juu ya furaha, wakati mtu akielekea kukata tamaa na mara unatokea mwaka na kuondoa giza lote. Ni shukrani kwa Mungu. Hapa tunaona ni kwa namna gani muda unakuwa mfupi wa kusubiri, na hali ya kukosekana kwa uvumilivu ambayo iligubikwa kwa kusubiri! Zakaria inazungumzia ukweli ambao ushakamilika!

Zakaria anajua fika kwamba Umwilisho ushakamilia. Hii inajidhihirisha kwa maneno yake ya mkazo katika utenzi wake; 'amekuja kuwakomboa, amekwisha kukombolewa, alimfufua' ni Nabii, kuashiria uhakio lijalo. Zakaria atakuwa anajua pia Famili ya Kifalme ya Maria kwa asili, kwa namna anavyo sema juu ya 'mlango wa Daudi.' “Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake,” Lk 1:69

'Pembe' ya wokovu ni nembo iliyo chukuliwa kutoka wanyama, na ina maanisha nguvu. Maneno haya yanakumbuka unabii kadhaa, na kama wajibu na utambulisho wa Masihi, vivuli na ushindi mkuu, ni kwa ajili ya ukombozi kwa watu wake. Maono yaliyo mbele ya Zakaria ni yale ya umshindi wa Mfalme Daudi uliotabiriwa kwa muda mrefu na manabii, ambao utaiweka Israeli huru kutoka maadui na wakandamizaji wake wa kigeni, ikiwa ni pamoja na dola ya  Kirumi. Hivyo ni Mungu mwenyewe ataye watembelea na kuwaokoa watu wake. “Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,” Lk 1:74.

Kuna aina mbili za kutembelewa katika hali ya Kimungu, moja ikiwa kwa huruma na nyingine kwa hukumu. Wazo la wokovu Kimasiha limeelezwa kwa upana na kuinuliwa vya kutosha katika sehemu hii ya Injili, Lk 1:71-Lk 1:75.  Neno 'ukombozi' limeelezewa vizuri kama ilivyo kwa maelezo ya 'pembe ya wokovu.' Ukombozi umebeba masuala mazito ambayo pia huonekana ni makusudi ya Mungu. Jambo hili hujionyesha katika hali tatu zilizofungamana: kwanza, kwa kuonyesha huruma kwa Mababa  waolikufa kutokana na safari hii katika historia ya wokovu.  Hili ni wazo kuu, na mwono utokao hapa kama pumziko lililotukuka na lenye heshima ya juu kabisa. Tendo hili laonyesha wakishiriki katika furaha ya kuja kwake Masiha, na pengine katika baraka ambazo Yeye, Masiha anazileta. Hali hii ni zaidi ya lugha ya picha. Ni zaidi ya yale yanayoweza kufikirika.

Suala la pili ni kukumbukwa kwa ahadi zake Mungu, au kwa maneno mengine, kutimizika kwa ahadi zake. Mwisho ni kwamba taifa lililowekwa huru, lazima limtumikie Mungu. “Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu, Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote,” Lk 1:74-75. Ukombozi wa nje ulikuwa mbele ya macho ya watu watauwa kama Zakaria ambao ushirika wao ulikuwa kama njia mojawapo ya kufikia mwisho. Uhuru wa kisiasa ulikuwa lazima kwa utumishi wa Mungu, na ulithaminiwa hasa kama kielelezo cha kufikia hazma hiyo. Katika Utenzi huu, Zakaria unaibua mambo muhimu sana ambayo wana wa Israeli hawakuwa huru kuyafanya ndani ya dola zile za kigeni. Hivyo, 'uhuru wa kuabudu Mungu,' na Mungu kuabudiwa’ ni moja mtazamo wa Zakaria kuhusu nyakati za Kimasiha, Lk 1:74-75.

Ukitazama matumizi ya neno huduma ya kikuhani, Kuhani Zakaria hajasahau kwamba kwa kadiri ya mwongozo na mtazama wa awali, Waisraeli wote walikuwa Taifa la Makuhani. Kwa mtazamo huu, naye Zakaria anamatazamio hayo yenye kuelekea ukamilisho wa jambo hili, na uwezekano wa kubadilishwa kwa mpango wake katika ukuhani kwa wote. Kwa maana nyingine Zakaria hajui kwa kina ukweli anaouimba. Mwisho wa kuja kwake Kristo, na wa ukombozi ambayo Yeye anafanya kwa ajili yetu kutoka mikono ya adui zetu, ukweli huu hauwezwi kusema vizuri zaidi ya maneno haya. ‘Tunakombolewa ili tupate kuwa makuhani kwa Mungu na kwa Mungu.’

Huduma yetu ya kikuhani lazima itolewe katika 'utakatifu na haki,' katika kuwekwa wakfu kwa Mungu na utekelezaji wa majukumu yote. Hivyo haipaswi kuingiliwa au kuwa huduma ya mara chache, kama Zakaria, ambayo alihudumu  wiki mbili katika mwaka. Hata hivyo utenzi  huu wa Zakaria waweza kuwa umeanza kwa wazo la nje la kuokoa la Kimasiha. Hata hivyo wazo hili laonyesha kwenda mbali zaidi ya kile kisemwacho katika utenzi huu. Tunaweza kujifunza kutoka ‘kuhani-nabii,’ ambaye hali hii inatabiri juu ya watu wale wenye hekima, ‘mamajusi’ na kuleta sadaka zao kwa  Kristo ambaye bado kuzaliwa. Tendo hilo pia linatoa tafsi ya “nini kuhusu wokovu wa kikristo,” na “kwa nini unatolewa kwetu.”

Kuna kitu ambacho kipo wazi na hai kuhusu mtoto ambaye ameweka yote  yasiyojulikana katika mikono ya mama yake. Tofauti kati ya yeye kama yeye na kazi ambayo inamsubiri, ubaba wa ajabu na furaha ambayo bado kueleweka juu ya mtoto, na dhana yake katika miaka ijayo, na kwenda kama mpiga mbiu-mbele ya Bwana inajidhihirisha. Hivyo ni vyema kufahamu uzito wa ufahamu wa kinabii katika kazi ya Yohana. Yohana Mbatizaji 'aliandaa njia' kwa kufundisha kwamba 'ukombozi' wa kweli ambao hukuwa kwa kupatikana tu ukombozi kutoka dola Kirumi, bali pia 'ondoleo la dhambi.' Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao,” Lk 1:76.

Hivyo Yohana Mbatizaji hakutoa tu 'maarifa ya wokovu,' katika maana ya kutatolewa kwa wokovu huo, bali pia kwa maana ya ufahamu wa nini kuhusu wokovu huo au kinachojumuisha maana nzima ya wokovu. Yohana Mbatizaji hakuwa mhubiri wa uasi, kama misukosuko na machafuko kama wazalendo wa siku zake walivyokuwa wakipendelea yeye afanye, bali alikuwa mhubiri wa toba ya kweli. Kazi yake ilikuwa kuamsha ufahamu kuhusu dhambi, na hivyo kuwasha tamaa ya kweli juu ya wokovu na ukombozi kutoka dhambi, ambayo ndiyo utumwa uliowatumikisha watu. Zakaria ' asiye na lawama' aliona utumwa wa kweli ulioutumikisha Taifa lake, na nini maana ya kazi ya wokovu ikiwa ni pamoja na kauli mbiu yake. Tunahitaji daima kukumbushwa ukweli kwamba wokovu wa pekee na ukombozi ambayo unaweza kutufanya sisi kuwa wema unahusu kuondokana na hali ya dhambi  kwa msamaha na kwa utakatifu, na hivyo kutoka katika kongwa la dhambi.

Maneno yanayoufunga utenzi huu wa Zakaria, “Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani,” Lk 1:79, yafungua baraka na neema kwa watu wote wenye hofu ya Mungu na wanaoishi katika kweli na haki. Hivyo kumjua Mungu kupitia  marafiki zetu, ni pamoja na kupatanishwa nao kwa hali zote. Kuwa rafiki ya watu wote, ni amani. Hivyo njia ya kuelekea heri hiyo inaonyeshwa kwetu kwa jua la haki ambao upendo wa moyo wa Mungu ametumwa katika kuleta mwanga.  Hakuna shaka kwamba Zakaria anaona kwa undani zaidi ukombozi ambao Kristo angeuleta kuliko kuvunjwa kwa ukomo wa kifungo cha  kidunia.

Tumsifu Yesu Kristo!

“Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza,” Kut 15:2

Tusali:-Ee Yesu na Mkombozi wetu, tuongoze mara zote katika mwanga wako. Amina

No hay comentarios:

Publicar un comentario