SIKUKUU
YA MTAKATIFU BARTOLOMEYO, MTUME
Somo: Ufu 21:9-14
Zab/Kit: 145:10-11,
12-13, 17-18
Injili: Yoh 1:45-51
Nukuu
“Upande
wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande
wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu,” Ufu 21:13
“Na
ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina
kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo,” Ufu 21:14
“Nathanaeli akamwambia,
Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone,” Yoh 1:46
“Nathanaeli akamjibu,
Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli,” Yoh 1:49
“Yesu
akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini?
Utaona mambo makubwa kuliko haya,” Yoh 1:50
“Akamwambia,
Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea
na kushuka juu ya Mwana wa Adamu,” Yoh 1:51
TAFAKARI: “Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia,
Njoo uone.”
Wapendwa wana wa Mungu, wale wote waliotukuzwa na Mungu na kuinuliwa
juu kabisa hawakuwa watu wa pekee sana katika jamii. Tabia ya Mungu katika
kuonyesha ukuu wake uviinua vilivyo dhauriwa katika jamii na kuvidondosha
vinavyojikweza mbele za watu. Maandiko Matakatifu yanafunua ukweli huu kwa
mifano mingi sana. Kwa ukaribu katika kweli hii tumtazame Mama yetu Bikira
Maria. Kwa ushuhuda wa makuu ya Mungu, Mama Bikira Maria asema, “amefanya nguvu
kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
Amewaangusha wakuu katika viti vyoa vya enzi; Na wanyonge amewakweza,” Lk
1:51-52. Huyu ndiye Mungu asiyewatupa wanyonge na wale wote
wenye kumcha.
Wapendwa wana wa
Mungu, leo Mama Kanisa anavyo sherehekea sikukuu ya Mtakatifu Bartolomeyo
Mtume, nasi tunapewa nafasi ya kuutafakari upendo wa Mungu usio na upendeleo.
Yesu hakuwachagua watu wa pekee sana ili wafanya yale aliyotaka wafanye, yaani,
kuieneza kauli mbiu yake ‘ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini
Injili,’ Mk 1:15. Badala yake aliwachagua watu wa kawaida kabisa na wengine
walikuwa na mwonekano mbaya katika jamii kama Mathayo karani, Mt 9:9. Mitume
hawakuwa na elimu ya pekee sana. Wengi wao walikuwa wavuvu tu.
Ndugu yangu, kitu cha kutazama siyo mtu kadiri
ya mwonekano wake nan je na mbwembwe zake, bali neema ile ifanyayo kazi ndani
yake. Ndiyo kwa maantiki hii utume kwa Mitume unafananishwa kama Bibi Harusi
aliyeshuka kutoka mbinguni kama mji wa Yerusalema. Mji huu una milango mitatu pande zote nne,
yaani, kaskazini na mashariki, na kusini na magharibi, Ufu 21:13. “Na
ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina
kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo,” Ufu 21:14.
Katika Injili ya leo tunaona Mitume hawa
kuchakuguliwa kwao hakukua swala la kubahatisha. Yesu Kristo alifanya hivyo na
kumaanisha hivyo katika uchaguzi wake. “Filipo
akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika
torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti,” Yoh 1:45.
Nathanaeli hakusadiki kweli hiyo, na badala yake aliyashikilea mapokea ya agano
la kale na kumwambia Filipo, “Laweza neno jema kutoka Nazareti?” Yoh
1:46a. Filipo aliye jaa Imani na Matumaini kwa kile alichokishuhudia akamjibi,
“Njoo uone,” Yoh 1:46b.
Ndugu yangu, Yesu anapokutembelea huwezi
kubaki kama ulivyokuwa mwanzo. “Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u
Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli,” Yoh 1:49. Hata kwa jibu hili la kina
la Nathanaeli, Yesu anataka Nathanaeli ajue zaidi ukweli kuhusu Yesu Kristo. “Yesu
akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini?
Utaona mambo makubwa kuliko haya,” Yoh 1:50. TUKIWA NDANI NA KATIKA YESU,
tutayaona mengi. Naye Yesu anatuambia, “Mtaziona mbingu zimefunguka
na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu,” Yoh 1:51. Huu
ndio utukufu wa Yesu utakao dhihirishwa kwa wale wote wamchao.
Tumsifu Yesu Kristo!
“Utaona mambo makubwa kuliko haya,”
Yoh 1:50b
Tusali:-Ee Yesu tujalie imani
dhabiti kama ya Mitume wako. Amina
Mtakatifu Bartolomeyo, Mtume,
Utuombee
No hay comentarios:
Publicar un comentario