SIKUKUU YA MTAKTIFU LUKA, MWINJILI
Somo:
2Tim 4:10-17b
Zab/Kit: 145:10-11, 12-13, 17-18
Injili: Lk 10:1-9
Nukuu:
“Katika
jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote
waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo, ili kwa kazi yangu ule
ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa
katika kinywa cha simba,” 2Tim 4:16-17b
Mavuno
ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno
apeleke watenda kazi katika mavuno yake,” Lk 10:2
“Basi,
kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi
amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba
hii,” Lk 10:7
“Na
mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele
yenu; waponyeni wagonjwa waliomo,
waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia,” Lk 10:8-9
TAFAKARI:
“Kuishi na kuuhubiri Ufalme wa Mungu.”
Wapendwa katika Kristo,
leo Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Mtakatifu Luka Mwinjili. Kama jumuiya ya wenye
hofu ya Mungu, Yesu anatualika kuliomba hili kadiri ya maitaji ya kanisa lake,
na kusema, “Mavuno ni mengi,
lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda
kazi katika mavuno yake,” Lk 10:2. Hili ni jukumu la kila mbatizwa.
Kufikia
lengo la kuutangaza ufalme wa Mbinguni kwa wengine kama alivyofanya Mwinjili
Luka, sisi tuliopata habari hii ya wokovu yatupasa kulisimamia jambo hilo kwa
weledi mkubwa, kwa kuwa waaminifu kwalo, na kuushikila ukweli huu bila
kutetereka. Yesu anatutaka kuwa makini sana huko tuendako kuupeleka ujumbe wa
wokovu. Naye anasema, “Basi, kaeni katika
nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa
ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii,” Lk 10:7. Na
lifanyike jambo moja kwa wakati.
Hii
ni pamoja na kuwa makini kwa jambo lile lile tu. Tusibebe ajenda nyingi katika
safari hii ya uinjilishaji. Mambo hayo {mfuko, mkoba, viatu na wala kuwaamkie
mtu njiani} tukiambatana nayo yatatuchanganya na kutufanya tupoteze mwelekeo.
Tuambatane na kubeba yale tu tunayohitaji kwa utume huo. Tusipokuwa na uchache
wa vitu furaha na amani ya kweli hutoweka. Tusiuzunike pale ambapo tunaona
mambo hayakwenda kama tulivyotarajia. Kufanya hivyo ni kupoteza muda bure kwani
muda hautungoji hata kidogo.
Katika
jambo hili Yesu anasema, “Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi,
tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu
yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya
kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia,” Lk 10:10-11. Jambo la msingi la kuzingatia ni
kufanya yale tu tuliyotarajia kuyafanya na kuwa na mahusiano mazuri na wale
tuliokusudia kuwainjilisha neno la Mungu. “Na
mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele
yenu; waponyeni wagonjwa waliomo,
waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia,” Lk 10:8-9. Tuyafanyapo haya kwa
unyenyekevu bila kujibakiza huwa msingi wa furaha na Amani yetu.
Mtakatifu
Luka Mwinjili sifa yake ya pekee ni utayari wake wa kutoka nje ya mazingira
yake na kupeleka habari njema kwa mataifa. Ni Mwinjili pia ambaye kwa kiasi
fulani haionyeshi ubaguzi au upendeleo kwa dhima nzima ya historia ya wokovu wa
mwanadamu. Kwa upendo wake Mungu, na kwa vile tumeumbwa kwa sura na mfano wake,
wote tumeitwa kuurithi ufalme wa mbinguni. Na jambo hili linajidhihirisha
katika kweli hii, kwamba, “Katika jawabu langu la kwanza
hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe
hatia kwa jambo hilo, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu,
hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba,” 2Tim
4:16-17b. Safari ya uinjilishaji siyo lelemama. Ni kujitoa muhanga haswa na
bila kujibakiza.
Leo kwa kufuata nyayo
za Mtakatifu Luka Mwinjili, kila mbatizwa na mwimarishwa ni jukumu lake la
msingi pale alipo kufanya uinjilishaji mpya. Na yote tuyafanyayo yajengwa juu
ya msingi imara wa Kristo mwenyewe. Mimi na wewe tuliyebatizwa na kuimarishwa
tuwe chumvi na mwanga katika dhima hii mpya, yaani, uinjilishaji mpya pale
nilipo.
Tumsifu Yesu Kristo
“Na mji wo wote
mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni,
Ufalme wa Munguumewakaribia,” Lk 10:8-9
Tusali:-Ee
Yesu, tufanye vyombo vyako katika uinjilishaji mpya pale tulipo. Amina
No hay comentarios:
Publicar un comentario