JUMANNE
WIKI YA 15 YA MWAKA-C
Somo: Isa 7:1-9
Zab: 48:2-3a, 3b-4, 5-6, 7-8
Injili: Mt 11:20-24
Nukuu:
“Basi
Bwana akamwambia Isaya, Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana
wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja wa
dobi; ukamwambie, Angalia,
ukatulie; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga
hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa
Remalia,” Isa 11:3-4
“Ole wako, Korazini!
Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika
katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu,” Mt
11:21
“Walakini nawaambieni,
itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko
wewe,” Mt 11:24
TAFAKARI: “Itakuwa rahisi nchi ya Sodoma
kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.”
Wapendwa wana wa Mungu,
wahenge wanasema, ‘sikio la kufa halisikii dawa.’ Moja ya njia ya kukua kiroho na kimwili ni
kuuona uhalisia wa mambo kama ulivyo. Mtazamo huu upo hata kwenye maisha ya
kawaida ya kila siku. Ushabiki wa mambo unapozidi ukweli wa mambo, kifuatacho
ni kupiga jaramba la maendeleo pale pale ulipo huku ukijifariji kwa upumbavu.
Na heri aliye mjinga kwani upo uwezekano wa kujifunza na kuelewa kuliko kuwa
mpumbavu usiye tayari kujifunza kwa sababu wajifariji kujua usichokijua.
Jamii yoyote ile inayoghubikwa na upumbavu
itaichukuwa muda mrefu sana kuifikia kweli. Hata pamoja na giza hili, Mungu
hachoki kusimama katika kweli na haki kwa watu wake. Wapo kati yetu wausimamiao
ukweli na hata kuchukiwa na kundi hili kubwa la wapumbavu. Nabii Isaya ni mmoja
ya watu hayo waisimamiayo kweli. Naye anamwambia Mfalme Ahazi, “usiogope wala usife moyo,” Isa 11:4a. Lililo kweli na libaki
kama lilivyo na lisimamie hadi mwisho.
Mara zote tunapopambana na
kweli, au kujikwamua kwenye shida fulani, mawazo pingamizi hayakosekani. Ugumu
huu wakati mwingine husababishwa na kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa jambo
lile. Jambo hili ndilo analolisema Yesu anapoitazama miji ile iliyokithiri kwa
uovu. “Ole wako,
Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika
katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu,” Mt
11:21. Ni mara ngapi tunaambiwa ukweli wa mambo lakini mara zote tunabakia na
ushabiki usiokuwa na tija yoyote? Kwa nini hatupendi kuona ukweli kama ulivyo
na badala yake tunaupindisha? Katika jambo hili, Yesu anatupa angalizo na
kusema, “Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya
Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe,” Mt 11:24.
Wapendwa, hawatashuka malaika kutoka mbinguni na kutuambia
mambo haya zaidi ya watu wenye uelewa tunaoishi nao kila siku kutuambia kweli
hiyo. Mungu utumia watu wake
kulisemea lile lililo ovu. Watu wenye maadili mema na mwono chanya, walisemapo
jambo yatupasa kusikia na kulipembua kwa kina. Je, yote yasemwayo kuhusu maisha
yako, hali yako, na Taifa lako hayana ukweli? Je, unaridhika na hali hii?
Umechukua hatua yo yote?
Tumsifu Yesu Kristo!
“Ole wako, Korazini! Ole
wako, Bethsaida!” Isa
11:21a
Tusali:-Ee Mungu tupe nguvu ya kusimama katika kweli na haki
No hay comentarios:
Publicar un comentario