lunes, 11 de enero de 2016

TAFAKARI: JUMANNE WIKI 1 YA MWAKA-C

JUMANNE WIKI YA 1 YA MWAKA-C
12/1/2016
Somo: 1Sam 1:9-20
Zab: 1Sam 2:1, 4-7, 8abcd
Injili: Mk 1:21-28
Nukuu:
Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe,” 1Sam 1:11

Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba,” 1Sam 1:17

Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena,” 1Sam 1:18

Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka,” 1Sam 1:19

Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana,” 1Sam 1:20

Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi,” Mk 1:22

Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?” Mk 1:23-24

Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke,” Mk 1:25

Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!” Mk 1:27

TAFAKARI: “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Kuwa na Imani.”

Wapendwa wana wa Mungu,  Mungu wetu sio Mungu wa kushindwa hata kidogo. Kwa maneno mengine, Mungu ninaye mwamini hawezi kuliumba jiwe kubwa kiasi chochote kile unachoweza kufikiria alafu ashindwe kulibeba jiwe hilo. Huyo siye Mungu ninayemwamini! Je, waamini Mungu anaweza?

Kwa imani aliyokuwa nayo Hana na nadhiri aliyoweka juu ya mtoto yule aliyemwomba Mungu, yote yanatendeka. Nadhiri awekayo mtu kwa kile aombacho ndiyo dhamiri ibebayo kile aombacho. Mara nyingi tunaomba na hatupati kwa sababu dhamiri iliyondani yako ni mbaya hata kama kile uombacho kwa mtazamo wa nje ni kizuri. Na hii ndiyo sababu anayotupa Mtume Yakobo kwa nini hatujibiwi maombi yetu. Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu,” Yak 4:3. Dhamiri ya Hana kwa kile aombacho ni njema na nzuri machoni mwa Mungu. Hana Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe,” 1Sam 1:11

Hata hivyo Mungu hutumia mambo yale yale ya kawaida kadiri ya hali zetu, mazingira na uwezo wetu kutenda Makuu yake wetu tunapojiachia kwake pasipo shaka. Hivyo, Eli Kuhani, alipowapa baraka Hana na Mumewe, wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka,” 1Sam 1:19. Ikiwa uliweka nadhiri kwa Mungu na ukafanikiwa kile ulichokiomba, yakupasa kufanya kadiri na ahadi yako. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana,” 1Sam 1:20.

Wapendwa wana wa Mungu, uwepo wa Kristo katika maisha yetu umetuweka karibu sana na Mungu naye ndiye Mungu. Alitamkalo Yesu limejaa mamlaka yote kwani ni neno aliyemwilishwa. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi,” Mk 1:22. Litamkwapo jina la Yesu hakuna nguvu yoyote ile na hasa nguvu za giza zinazoweza kustahimili jina hili Tukufu kupita majina yote. Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?” Mk 1:23-24. Nguvu na Utukufu wa Kristo hata pepo wachafu wanajua na kukiri. Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke,” Mk 1:25.

Nguvu na Mamlaka aliyo nayo Kristo Yesu, hakuna chochote tutakachomwomba kwa imani na dhamiri njema aache kutupatia. Na yote hayo huyafanya kadiri ya mapenzi yake na mahitaji yetu. Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina,” Rum 16:27. Ukweli huu unathibitika ndani ya sinagogi alivyokinyamazisha kichwa cha pepo mchafu na kuamuru amtoke mtu yule. Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!” Mk 1:27. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Kuwa na Imani.

Tumsifu Yesu Kristo!


Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina,” Rum 11:36

No hay comentarios:

Publicar un comentario