JUMAMOSI WIKI YA 1 YA MWAKA-C
16/1/2016
Somo: 1Sam 9:1-4, 17-19; 10:1
Zab: 21:2-3, 4-5, 6-7
Injili: Mk 2:13-17
Nukuu:
“Basi, kulikuwa na mtu
mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori,
mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye
nguvu,” 1 Sam 9:1
“Naye alikuwa na
mwana, aliyeitwa jina lake Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa
Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa
mrefu kuliko watu wote,” 1 Sam 9:2
“Hata Samweli
alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu
ndiye atakayewamiliki watu wangu,” 1Sam 9:17
“Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina
kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya
watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui
zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu
ya urithi wake,” 1Sam 10:1
“Hata alipokuwa
akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate.
Akaondoka akamfuata,” Mk 2:14
“Hata alipokuwa
ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi
pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata,” Mk 2:15
“Na waandishi na
Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi,
waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye
dhambi?” Mk 2:16
“Yesu aliposikia
aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita
wenye haki, bali wenye dhambi,” Mk 2:17
TAFAKARI: “Sikuja kuwaita wenye haki,
bali wenye dhambi.”
Wapendwa wana wa Mungu, utabiri wa malaika juu ya kuzaliwa
kwa Yesu, uliweka wazi juu ya kile anachokijia Yesu katika ulimwengu huu.
Malaika Gabriel anamtoa hofu Yusufu mume wa Bikira Maria juu ya mimba ile kwani
Yusufu alikuwa mtu wa haki na hakupenda makuu. Hivyo njia ya pekee ni kumwacha
kimya kimya mkewe. Malaika akamwambia Yusufu, “Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu
kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye
ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao,” Mt 1:20-21. Hivyo Yesu
anathihirisha ukweli huu katika Injili ya leo wakati Mafarisayo wanapowashambulia
wanafunzi wa wake kuona Yesu anakula na watoza ushuru na wenye dhambi. “Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali
walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi,” Mk 2:17. Kristo
amekuja na yupo muda wate kutupatanisha na Mungu Baba. Kristo kwetu leo ni
daraja imara kuelekea uzima wa milele.
Hakuna
hata mmoja kati yetu asiyehitaji huruma, msamaha, na upendo wa Mungu. Hata kama
twajiona wenye haki na wasio na hatia, bado tunaitaji upendo wa Mungu. Pendo
lake Yesu utuvutia tuwe wake milele. “Nami naliwajulisha
jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani
yao, nami niwe ndani yao,” Yoh 17:26. Hivyo uwe una afya ya mwili na roho, au
hauna afya hiyo bado wahitaji pendo la Mungu.
Basi
wapendwa wana wa Mungu, tusipoteze muda mwingi kuzichunguza dhambi za watu kama
walivyopoteza muda huo Mafarisayo na kusahau wongofu wao wenyewe. Yesu anasema
hili juu ya yeyote yule mwenye kupoteza muda wake kwa kuzitazama dhambi za
mwenzake bila kuhangaikia wongofu wake mwenyewe. “Mnafiki wewe, itoe
kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa
kile kibanzi katika jicho la ndugu yako,” Mt 7:5. Ninapogundua mwenzangu
kaanguka katika dhambi tendo lile liwe kioo cha kujitazama kwanza ndani ya
nafsi yangu kabla ya kuhukumu. Tendo hilo liwe kielelezo cha mimi kuiona huruma
ya Mungu ndani yangu na kwa yule aliyedondoka katika dhambi. Na mara zote
nionapo tendo hilo nijiulize hivi; “ya mwenzangu yamejulikana, yangu
yamesitiriwa kwa muda tu, yanipasa kutubu.”
Tusipoona
na kuonja huruma ya Mungu ndani ya nafsi zetu na kwa wenzetu, hatuwezi kukua
kiroho. Nisipoonja hali hii ndani yangu, ukristo wangu na huduma niitoayo haina
maana yoyote zaidi ya uigizaji tu.
Huruma na upendo wa Mungu wajidhihirisha pia katika somo letu la kwanza juu ya
Sauli Mfalme mteule. Pamoja na yote mabaya yaliyofunuliwa juu yake, bado Mungu
anaruhusu awe Mfalme na kuitenda kazi yake. “Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina
kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya
watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui
zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu
ya urithi wake,” 1Sam 10:1. Je, waweza
mkabidi mtoto wako simba mwenye njaa? Mungu hufanya bila shaka yoyote.
Tumsifu
Yesu Kristo.
“Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira,
ni mwingi wa rehema,” Zab 145:8
No hay comentarios:
Publicar un comentario