ALHAMISI, SIKU 24 YA MAJILIO MWAKA-C
24/12/2015
Somo: 2Sam 7:1-5, 8b-11, 16
Zab: 88:2-3, 4-5, 27, 29
Injili: Lk 1: 67-79
Nukuu:
“Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake? Nalikutwaa katika zizi la kondoo,
katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli,” 2Sam
7:5b
“nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia
mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu
walioko duniani,” 2Sam 7:9
“Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami
nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa
uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza,” 2 Sam 7:10
“Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake,
na kuwakomboa,” Lk 1:68
“Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia,” Lk
1.71
“Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na
kumwabudu pasipo hofu,” Lk 1:74
“Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia
mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Uwajulishe watu wake
wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao,” Lk 1:76
“Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza
miguu yetu kwenye njia ya amani,” Lk 1:79
TAFAKARI: “Kwa kuwa amewajia watu
wake, na kuwakomboa.”
Wapendwa wana wa Mungu, kinachogusiwa katika somo letu la
kwanza ni yale yaliyojiri katika nyakati za mwisho za Mfalme Daudi. Ufalme wake
katika miaka yake hiyo ya mwisho ulikuwa imara na watu wake walifurahia amani
ya kweli. Licha ya kwamba Mfalme Daudi alimiliki jumba zuri la kifalme alikosa
nyumba ya heshima kwa ajili ya kuhifadhi sanduku la agano. Nabii Nathani
anamkumbusha wajibu huo muhimu wa kufanya Mfalme. Ujumbe wa Mungu kwa Mfalme
Daudi ulisema hivi, “Je!
Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake? Nalikutwaa
katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu
wangu, juu ya Israeli,” 2Sam 7:5b. Ujumbe huu ulimtaka Mfalme Daudi kwa ukarimu
wake uwe kigezo pia cha kuona ukarimu wa Mungu. Hivyo yampasa kufanya kitu
kuhusu Sanduku lile la Agano lihifadhiwe mahali pazuri zaidi. Yatupasa kuwa
wakarimu zaidi kwani kwa uwepo wetu duniani hapa ni ukarimu mkubwa sana wa
Mungu.
Hivyo agano liliwekwa katika mlima sinai linawekwa katika
uhalisia wake. Ujumbe huu pia unahusisha yaliyosema na Nabii Isaya, 9:6, kwa kuzaliwa
mtoto na mfalme wa Amani, na uokoaji wake, Lk 1:32, 69, kwa kupewa kiti cha
Baba yake Daudi na kuwa pembe ya wokovu. Hivyo Masiha atakuwa mtoto wa Daudi,
na ufalme wake utakuwa ufalme wa milele. Undani wa habari hii tunakutana nao
katika utenzi wa Zakaria uliobeba Injili yetu ya leo.
Wapendwa wana wa Mungu, “Zakaria akajazwa
Roho Mtakatifu, na kutoa unabii.” Maneno haya yanaonekana kutumika katika
maana yake pana ya uhihisho utamkwao
katika hali ya kupongeza na sifa juu ya makuu mtu aliyotendewa na yenye
kustaajabia. Mfano wa hali hii tunakutana nayo (katika kitabu cha kwanza cha
Samueli 19:20; na waraka kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho 14: 24-25).
Utenzi au wimbo huu wa Zakaria
unaonekana kama taarifa iliyoandikwa, pengine, na Zakaria mwenyewe, kwa kusifu
mara maada ya kurudishiwa uwezo wake wa kuongea tena.
Maneno katika utenzi huu yawezekana ni
tafakari aliyokuwa nayo kipindi kizima cha yeye kutokuongea. Ni tafakari
iliyozama ndani kabisa katika matendo Makuu ya Mungu kwake na kwa Taifa zima la
Israeli. Utenzi wenyewe wa Zakaria ndio uliobeba Ijili yetu ya leo. Ni vyema
tukatafakari kwa undani juu ya utenzi huu, Lk 1:67-80.
Zakaria alikuwa bubu alipoacha kuamini
ujumbe ule wa Malaika juu ya uwezo wa Mke wake kuzaa. Ububu wa Zakari ni
matokeo ya kutokuamini makuu ya Mungu. Midomo yake ikafunguka wakati
alipoamini. Zakaria ni wa mwisho kati ya Manabii wa Agano la Kale, ingawa
Yohane yeye alikuja kukaribisha Angano Jipya. {Mathayo 11: 9 - Mathayo 11:11}
Kwa maana hiyo, Zakaria alikuwa nabii wa mwisho wa mpango wa Agano la Kale,
kabla ya kuja kwa mtoto wake kwa kuhusisha Agano la Kale na Agano Jipya],
aliyekuwa karibu sana na kuja kwake Masiha.Wimbo wa Zakaria unachukua Mwangwi
wa zamani zote, na kuviyeyusha ndani ya mwanga mpya wa matumaini.
Utenzi au wimbo huu wa Zakaria tunaweza
kuugawa katika sehemu kuu matatu: sehemu ya kwanza ni {Luka 1:68 - Luke 1:75},
habari tukutanayo hapa ni kuhusu adhimisho la
kuja kwa Masihi, kwa namna ya pekee katika kuikomboa Israeli kutoka
maadui zake. Sehemu ya pili ni {Luka
1:76 Luka 1:77}, habari za sehemu hii zipo katika lugha ya picha zaidi juu ya
sintofahamu ya huyu ‘mtoto’ Yohane. Na sehemu ya tatu na ya mwisho, {Luke 1:78
- Luke 1:79}, inaturudisha katika wazo msingi kuhusu Masiha, lakini sasa
linagusa juu ya suala la kuja kwake kama Mwanga kwa wote wanaokaa katika giza.
Kama tunakumbuka kwamba miaka mia nne ya
sintofahamu juu ya Taifa hili la Israeli, kwa sehemu kubwa Waisraeli walikuwa
chini ya mateso na dola ya kigeni, ilikuwa imepita tangu mwisho wa
Manabii. Hivyo kwa wakati huo wote macho yao mchana na usiku
yalionekana kunyong'onyea kwa kumsubiri
Masiha aliyeahidiwa. Katika mazingira haya na ishara zilizokuwa zinaambatana na
tukio hili, ni wazi sasa tunaweza kuona yaliyokuwa yameujaza moyo wa Zakaria.
Ni wazi kwa ishara hizo saa imewadia, na kwamba mtoto hivi karibuni kuzaliwa
atatimiza ahadi ya Mungu na kukidhi matumaini yake yaliyoanza kutoweka.
Si ajabu kwamba maneno yake ya kwanza ni
mpasuko wa baraka za 'Mungu kwa wa
Israeli.' “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na
kuwakomboa,” Lk 1:68. Haya ni matamshi yaliyo bora na ya hali ya juu ya furaha,
wakati mtu akielekea kukata tamaa na mara unatokea mwaka na kuondoa giza lote.
Ni shukrani kwa Mungu. Hapa tunaona ni kwa namna gani muda unakuwa mfupi wa
kusubiri, na hali ya kukosekana kwa uvumilivu ambayo iligubikwa kwa kusubiri!
Zakaria inazungumzia ukweli ambao ushakamilika!
Zakaria anajua fika kwamba Umwilisho
ushakamilia. Hii inajidhihirisha kwa maneno yake ya mkazo katika utenzi wake;
'amekuja kuwakomboa, amekwisha kukombolewa, alimfufua' ni Nabii, kuashiria
uhakio lijalo. Zakaria atakuwa anajua pia Famili ya Kifalme ya Maria kwa asili,
kwa namna anavyo sema juu ya 'mlango wa Daudi.' “Ametusimamishia
pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake,” Lk 1:69
'Pembe' ya wokovu ni
nembo iliyo chukuliwa kutoka wanyama, na ina maanisha nguvu. Maneno haya
yanakumbuka unabii kadhaa, na kama wajibu na utambulisho wa Masihi, vivuli na
ushindi mkuu, ni kwa ajili ya ukombozi kwa watu wake. Maono yaliyo mbele ya
Zakaria ni yale ya umshindi wa Mfalme Daudi uliotabiriwa kwa muda mrefu na
manabii, ambao utaiweka Israeli huru kutoka maadui na wakandamizaji wake wa
kigeni, ikiwa ni pamoja na dola ya
Kirumi. Hivyo ni Mungu mwenyewe ataye watembelea na kuwaokoa watu wake. “Ya kwamba
atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,” Lk
1:74
Kuna aina mbili za kutembelewa katika hali
ya Kimungu, moja ikiwa kwa huruma na nyingine kwa hukumu. Wazo la wokovu
Kimasiha limeelezwa kwa upana na kuinuliwa vya kutosha katika sehemu hii ya
Injili, Lk 1:71-Lk 1:75. Neno 'ukombozi'
limeelezewa vizuri kama ilivyo kwa maelezo ya 'pembe ya wokovu.' Ukombozi
umebeba masuala mazito ambayo pia huonekana ni makusudi ya Mungu. Jambo hili
hujionyesha katika hali tatu zilizofungamana: kwanza, kwa kuonyesha huruma kwa
Mababa walikufa kutokana na safari hii
katika historia ya wokovu. Hili ni wazo
kuu, na mwono utokao hapa kama pumziko lililotukuka na lenye heshima ya juu kabisa.
Tendo hili laonyesha wakishiriki katika furaha ya kuja kwake Masiha, na pengine
katika baraka ambazo Yeye, Masiha anazileta. Hali hii ni zaidi ya lugha ya
picha. Ni zaidi ya yale yanayoweza kufikirika.
Suala la pili ni kukumbukwa kwa ahadi zake
Mungu, au kwa maneno mengine, kutimizika kwa ahadi zake. Mwisho ni kwamba taifa
lililowekwa huru, lazima limtumikie Mungu. “Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui
zetu, Na kumwabudu pasipo hofu, Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote,” Lk
1:74-75. Ukombozi wa nje ulikuwa mbele ya macho ya watu watauwa kama Zakaria
ambao ushirika wao ulikuwa kama njia mojawapo ya kufikia mwisho. Uhuru wa
kisiasa ulikuwa lazima kwa utumishi wa Mungu, na ulithamiwa hasa kama kielelezo
cha kufikia hazma hiyo. Utenzi huu Zakaria unaibua mambo muhimu sana ambayo
wana wa Israeli hawakuwa huru kuyafanya ndani ya dola zile za kigeni. Hivyo,
'uhuru wa kuabudu Mungu,' na Mungu kuabudiwa’ ni moja mtazamo wa Zakaria kuhusu
nyakati za Kimasiha, Lk 1:74-75.
Ukitazama matumimizi ya neno huduma ya
kikuhani, Zakaria, kuhani hajasahau kwamba kwa kadiri ya mwongozo na mtazama wa
awali, Waisraeli wote walikuwa Taifa la Makuhani. Kwa mtazamo huu, naye Zakaria
anamatazamio hayo yenye kuelekea ukamilisho wa jambo hili, na uwezekano wa
kubadilishwa kwa mpango wake katika ukuhani kwa wote. Kwa maana nyingine
Zakaria hayajui kwa kina ukweli anaouimba. Mwisho wa kuja kwake Kristo, na wa
ukombozi ambayo Yeye anafanya kwa ajili yetu kutoka mikono ya adui zetu, ukweli
huu hauwezwi kusema vizuri zaidi ya maneno haya. Tunakombolewa ili tupate kuwa
makuhani kwa Mungu na kwa Mungu.
Huduma yetu ya kikuhani lazima itolewe
katika 'utakatifu na haki,' katika kuwekwa wakfu kwa Mungu na utekelezaji wa
majukumu yote. Hivyo haipaswi kuingiliwa au kuwa huduma ya mara chache, kama
Zakaria, ambayo alihudumu wiki mbili
katika mwaka. Hata hivyo utenzi huu wa
Zakaria waweza kuwa umeanza kwa wazo la nje la kuokoa la Kimasiha. Hata hivyo
wazo hili laonyesha kwenda mbali zaidi ya kile kisemacho katika utenzi huu.
Tunaweza kujifunza kutoka ‘kuhani-nabii,’ ambaye hali hii inatabiri juu ya watu
wale wenye hekima, ‘mamajusi’ na kuleta sadaka zao kwa Kristo ambaye bado kuzaliwa. Tendo hilo pia
linatoa tafsi ya “nini kuhusu wokovu wa kikristo,” na “kwa nini ni unatolewa
kwetu.”
Kuna kitu ambacho kipo
wazi na hai kuhusu mtoto ambaye ameweka yote
yasiyojulikana katika mikono ya mama yake. Tofauti kati ya yeye kama
yeye na kazi ambayo inamsubiri, ubaba wa ajabu na furaha ambayo bado kueleweka
juu ya mtoto, na dhana yake katika miaka ijayo, na kwenda kama mpiga mbiu-mbele
ya Bwana inajidhihirisha. Hivyo ni vyema kufahamu uzito wa ufahamu wa kinabii
katika kazi ya Yohana. Yohane Mbatizaji 'aliandaa njia' kwa kufundisha kwamba
'ukombozi' wa kweli ambao hukuwa kwa kupatikana tu ukombozi kutoka dola Kirumi,
bali pia 'ondoleo la dhambi.' “Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana
utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Uwajulishe watu
wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao,” Lk 1:76.
Hivyo
Yohane Mbatizaji hakutoa tu 'maarifa ya wokovu,' katika
maana ya kutatolewa kwa wokovu huo, bali pia kwa maana ya ufahamu wa nini
kuhusu wokovu huo au kinachojumuisha maana nzima ya wokovu. Yohane Mbatizaji
hakuwa mhubiri wa uasi, kama misukosuko na machafuko kama wazalendo wa siku
zake walivyokuwa wakipendelea yeye afanye, bali alikuwa mhubiri wa toba ya
kweli. Kazi yake ilikuwa kuamsha ufahamu kuhusu dhambi, na hivyo kuwasha tamaa
ya kweli juu ya wokovu na ukombozi kutoka dhambi, ambayo ndiyo utumwa uliowatumikisha watu. Zakaria ' asiye na
lawama' aliona utumwa wa kweli ulioutumikisha Taifa lake, na nini maana ya kazi
ya wokovu ikiwa ni pamoja na kauli mbiu yake. Tunahitaji daima kukumbushwa
ukweli kwamba wokovu wa peke na ukombozi ambayo unaweza kutufanya sisi kuwa
wema unahusu kuondokana na hali ya dhambi
kwa msamaha na kwa utakatifu, na hivyo kutoka katika kongwa la dhambi.
Maneno yanayoufunga
utenzi huu wa Zakaria, “Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na
kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani,” Lk 1:79, yafungua baraka na neema
kwa watu wote wenye hofu ya Mungu na wanaoishi katika kweli na haki. Hivyo kumjua
Mungu kupitia marafiki zetu, ni pamoja
na kupatanishwa nao kwa hali zote. Kuwa rafiki ya watu wote, ni amani. Hivyo
njia ya kuelekea heri hiyo inaonyeshwa kwetu kwa jua la haki ambao upendo wa
moyo wa Mungu ametumwa katika kuleta mwanga.
Hakuna shaka kwamba Zakaria anaona kwa undani zaidi ukombozi ambao
Kristo angeuleta kuliko kuvunjwa kwa ukomo wa kifungo cha kidunia.
Tumsifu Yesu Kristo!
“Bwana ni nguvu zangu,
na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;
Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza,” Kut 15:2
No hay comentarios:
Publicar un comentario