JUMAMOSI WIKI YA 22 YA MWAKA-B
5/9/2015
Somo: Kol 1:21-23
Zab: 53
Injili: Lk 6:1-5
Nukuu:
“Na ninyi,
mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu
mabaya, amewapatanisha sasa; katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake,” Kol
1:21-22a
“Akawaambia, Mwana wa
Adamu ndiye Bwana wa sabato,” Lk 6:5
TAFAKARI: “Kristo katuweka huru, hivyo tusimame katika kweli kila
siku.”
Wapendwa wana Mungu, Kristo katuweka huru, hivyo tusimame
katika kweli kila siku. Kusimama katika kweli ni kuthamini na kuishi kweli ya
Mungu na kuwa na hofu yake. Hofu ya Mungu tuliyonayo msingi wake ni upendo wa
Mungu hasa kwa kumtoa mwanaye mpenzi kama sadaka, na kututoa kutoka utumwa wa
dhambi. Ukombozi wetu ni wa gharama kubwa sana. Je, wauthamini Ukristo wako kwa
kuishi Imani ya kweli? Mtume Paulo anatukumbusha habari hii kwa kusema, “Na ninyi, mliokuwa hapo
kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya,
amewapatanisha sasa; katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake,” Kol 1:21-22a.
Ni kwa
mantiki hiyo hapo juu kwamba Kristo ndiye kielelezo cha yote yale tuyafanyayo
ili tuurithi ufalme wa Mbingini tulioandaliwa na kuutamani. Je, yale yote
niyafanyayo leo na sasa yanaendana na sadaka ya Yesu pale msalabani? Yesu
anataka Wayahudi na wewe na mimi tuelewe kwamba yale tuyafanyayo yaendane na
thamani ya upendo wa Mungu kwetu, na Yeye, yaani Kristo ndiye msingi wa vyote.
Kristo akiwa msingi wa maisha yetu na sababu ya yale yote tuyafanyayo, basi
tutakuwa huru kweli kweli kwa sababu tutajua ni nini tunayemtumikia. Hivyo Yesu
anawaambia Wayahudi “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato,” Lk 6:5. Kristo ndiye mizania ya kweli kuhusu Mungu tunayemwamini
na kumwabudu. Kristo ndiye anayejua siri ya ufalme wa Mungu. Ndugu yangu Kristo
ndiye njia, kweli na uzima.
Tumsifu Yesu Kristo!
EE YESU KWAKO TU HURU.
No hay comentarios:
Publicar un comentario