IJUMAA WIKI YA 22 YA MWAKA-B
Somo: Kol 1:15-20
Zab: 99
Injili: Lk 5:33-39
Nukuu:
“Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na
vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi,
au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa
ajili yake,” Kol 1:16
“Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge
walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?” Lk 5:34
“Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya,” Lk
5:38
“Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa
kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema,” Lk 5:39
TAFAKARI: “Nguvu na mamlaka ya Kristo ni uthibitisho wa ujemedari
wake dhidi ya uovu.”
Wapendwa
wana wa Mungu, mamlaka aliyokuwa nayo Yesu ni vita dhidi ya uovu hapa duniani.
Ni ukweli usiopingika kwa kupitia jina lake tunapata uponyaji wa kweli. “Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini
nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama
uende,” Mdo 3:6. Mamlaka
ya Yesu yamejengwa chini ya mamlaka ya Mungu. Hivyo hakuna jambo lolote
alifanyalo Yesu Lisilo kuwa na uhusiano na Mungu, huku jambo lile likifunua
siri ya Mungu kila kukichwa. “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na
vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi,
au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa
ajili yake,” Kol 1:16. Kwa nini basi nakuwa na mashaka juu ya utendaji wa
Kristo katika maisha yangu?
Wapendwa
katika Kristo, Yesu anapotoa mfano wa vazi kuukuu na jipya, na kwa upande
mwingine divai ya zamani na kiriba cha kipya anataka kutufundisha jambo hili;
“kwanza kabisa lazima tujue sababu na malengo ya maisha yetu hapa tuniani.
Hatupo hapa duniani kwa bahati mbaya hata kidogo. Tupo katika ulimwengu huu
kadiri ya mpango wa Mungu ambao ni dhahiri na mathubuti. Hivyo lolote lile
lililo jema mbele ya Mungu huwiishwa na kufanya upya. Katika Injili ya leo
tunaona watu wakimletea Yesu malalamiko juu ya kufunga na kuomba. Kufunga kwetu
na kuomba kwetu uifaidia kwanza kabisa roho zetu na wenzetu. Tunawajibu huo
kiimani, na yatupasa kuutekeleza pasipo imani na msaada wowote. Ndiyo maana
Yesu anawauliza watesi wake swali hili: “Je!
Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?”
Lk 5:34. Maisha yapaswa kusherehekewa kwa sababu ni mali na zawadi ya Mungu.
Hivyo basi, upya wetu kiimani hutoshelezwa na upya
tuupokeao kwa Yesu tunaposhiriki masakramenti yake tukiwa katika hali ya usafi. Hivyo “divai
mpya sharti kutiwa katika viriba vipya,” Lk 5:38. Ndani na katika Kristo
kiimani hujengeka kwa matendo madogo madogo yanayompendeza Mungu. “Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani
divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema,” Lk 5:39. Ndugu
yangu ukiona vinaelea ujue vimeundwa.
Tumsifu Yesu Kristo!
EE YESU TUIMARISHE KATIKA IMANI. AMINA
No hay comentarios:
Publicar un comentario