IJUMAA WIKI YA 14 YA MWAKA-B
10/7/2015
Somo: Mwa 46:1-7, 28-30
Zab: 36
Injili: Mt 10:16-23
Nukuu:
“Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka
mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko,” Mwa 46:3
“Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona
uso wako, ya kuwa ungali hai,” Mwa 46:30
“Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu;
basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua,” Mt 10:16
“Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti
mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha,” Mt 10:21
“Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina
langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka,” Mt 10:22
TAFAKARI: “Mwenye kuvumilkia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”
Wapendwa wa Mungu, hakuna maisha mabaya kama maisha ya
kuishi na hofu. Hofu hudumaza akili zetu na kutufanya kutokuwelewa ukweli wa
maisha tunayoyaisha wakati wa sasa na wakati ule ujao. Mwenye hofu hawezi
kupanga sawasawa kuhusu maisha yake. Mbaya zaidi mtu yeyote mwenye kuishi
katika hofu, hali ile huwa kisababishi cha magonjwa mengine ya kiogani.
Yatupasa kuishinda hofu kila siku katika maisha yetu. Mungu wetu hapendi kamwe
tuishi katika hofu. Naye anasema, “Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri;
maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko,” Mwa 46:3. Maisha ni mtihani mkubwa
sana, ila yatupasa kuyaishi. Kuishi maisha haya yanatualika kufanya uthubutu.
Maisha ya
binadamu mwenye ufahamu wa kutosha hulenga hitimisho fulani. Maisha yenye
malengo ni taswira yenye umweleko chanya hata kama malengo yale hayajafikiwa.
Baada ya Israeli kumwona Yusufu anamwambia maneno haya: “Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya
kuwa ungali hai,” Mwa 46:30. Kila mmoja wetu hufurahia matunda ya kazi yake.
Kwa upande mwingine tunapokuwa tayari kutumika kwa ajili ya Kristo yatupasa
kuwa tayari kutaabika kwa ajili ya Kristo. Kuishi maisha yanayompendeza Kristo
ni kutangaza vita dhidi ya ufalme wa giza. Hivyo, “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi
iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua,” Mt 10:16. Ni katika
upole tunajifunza mambo mengi. Huu ndio upole wa hua. Ni katika busara
hufunuliwa yake yaliyojificha. Huku ni kuwa kama nyoka.
Kumfuata Yesu, kwatutaka kuikana nafsi, na hata wakati
mwingine kwenda kinyume na utaratibu tuliojijengea kutokana na mila na desturi
zetu. “Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na
baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha,” Mt 10:21. Kusalitiana huku kwa weza kutokea tunapoyaishi
yale Kristo anayotuwasa. Tunapofuata njia yake, kuishi ukweli wake, na kulishwa
uhai wake, wengi watatutenga. “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina
langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka,” Mt 10:22
Kufaulu
katika mtihani huu wa maisha ndani na katika Kristo kwa tutaka kuvumilia hadi
mwisho. Ni kuvumilia kwenye kutupa matumaini ya uzima wa milele.
Tumsifu
Yesu Kristo!
EE YESU TUPE UVUMILIVU.
No hay comentarios:
Publicar un comentario