ALHAMISI WIKI YA 15 YA MWAKA-B
16/7/2015
Somo: Kut 3:13-20
Zab: 104:1, 5, 8-9, 24-27
Injili: Mt 11:28-30
Nukuu:
“Mungu akamwambia
Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;
MIMI NIKO amenituma kwenu,” Kut 3:14
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha,” Mt 11:28
“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole
na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu,” Mt 11:29
“kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi,”
Mt 11:30
TAFAKARI:
“Utulivu wa kweli twaupata ndani na katika Kristo.”
Wapendwa
wana wa Mungu, kuzaliwa si lazima, ili kufa kama umeshazaliwa ni lazima. Ikiwa
tupo hai na tunaishi, hatuwezi kudumu katika hali hiyo siku zote bila kuwa na
mahangaiko. Binadamu huyapata mahangaiko yatokanayo na magonjwa, njaa, hali ya
hewa, na hata hali mbaya ya siasa. Hali mbaya ya siasi huwa pia chanzo cha
mahangaiko na kuwafanya watu kuwa wakimbizi katika inchi yao yenyewe, vifo vya
watoto, akina mama na watu wasio na hatia yoyote.
Ndugu
yangu, tunayaona mahangaiko pia kwa wana wa Israeli katika safari ya ukombozi
kutoka inchi Misri. Hivyo Musa anapopewa majukumu la kuliongoza Taifa hili
kutoka utumwani Misri, anataka kujua uhakika wa kile alichoambiwa na Mungu. “Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo
utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu,” Kut 3:14. Huyu
ndiye Mungu hai tunayemwamini na kumwabudu.
Leo kwa
yeyote yule mbatizwa na mwenye kumwamini Kristo, anapata kitulizo cha kweli
ndani na katika Kristo. Ni kupitia Kristo wote twaweza kuiona nuru na kuishi
katika nuru ya kweli. Hakuna jina lingine hapa dunia twaweza kuokolewa nalo nje
ya jina hili, Yesu Kristo. Yesu ndiye njia, kweli na uzima wetu. Yesu anasema, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye
kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha,” Mt 11:28. Kiboko cha mahangaiko yetu
kama watu waaminio na wafuasi wa Kristo ni Yesu mwenyewe. Mizigo yetu na taabu zake zote ni Kristo
mwenyewe anayeweza kutubebea tukiwa naye. “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha,” Mt 11:28.
Hakuna pumzisho la kweli nje ya Kristo. Mwongozo wa kweli katika mahangaiko
yetu ni Kristo mwenyewe. Mwongozo wake ni UPENDO, na hii ndiyo nira yake. “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa
mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu,” Mt
11:29. Ndugu yangu kwa nini hupendi kupenda?
Kwa nini humpendi huyo uliye weka mipaka naye? Je, Yesu angefanya hayo unayoyafanya?
Ndugu
yangu, ukipenda katika kweli yote, yote huwa mepesi. Kipimo cha kupenda
kinawiana na kipimo cha kusamehe. Usipo kuwa mwepesi wa kusamehe bado hujaijua
kweli ya Mungu. Katika hili Yesu anasema, “kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi,”
Mt 11:30. Ndugu yangu, ni mzingo upi ulio nao ni mzito ambao Yesu atashindwa
kuubeba?
Tumsifu Yesu Kristo!
EE YESU KRISTO, TUJALIE IMANI YA KWELI. AMINA.
No hay comentarios:
Publicar un comentario