JUMANNE WIKI YA 7 YA PASAKA-B
19/5/2015
Somo:
Mdo 20:17-27
Zab:
67
Injili:
Yoh 17:1-11a
Nukuu:
“Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu
hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji
hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja,” Mdo 20:22-23
“Lakini
siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo
wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya
neema ya Mungu,” Mdo 20:24
“Kwa
maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu,” Mdo 20:27
“Na
uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu
Kristo,” Yoh 17:3
“Mimi
nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio
wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao,” Yoh 17:9-10
“Wala
mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako,” Yoh
17:11a
TAFAKARI: “Uzima wa milele ndio huu; kumjua
Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo.”
Wapendwa wana wa Mungu, kila mmoja wetu hapa
duniani kaitwa kwa namna mbalimbali na ya pekee kadiri iliyompendeza Mungu.
Kuitwa huku na Mungu kwa itaji mwitikio wetu. Hivyo kila mmoja wetu
anavyoitikia bila kujibakiza ndivyo anavyojazwa uzima huo wa milele ambayo ni
tayari katika hatua, na ambao bado katika utumilifu wake. Hapa haijalishi
mwitikio huo umechukua taswira gani. Kwa maana nyingine haijalishi wewe ni
mlei, matawa, au mkleri. Hivyo basi, mwitikio huu lazima ulenge kumjua Mungu wa
pekee wa kweli, na Yesu Kristo.
Ni katika mwitikio huu kimaisha Mtume Paulo hajuutii
kumjua na kumtumikia Mungu aliye hai, na Yesu Kristo. Hivyo Mtume Paulo yupo
tayari kwa yote yatakayotokea kuhusu maisha yake na uhusiano wake na Mungu. “Basi sasa, angalieni,
nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo
yatakayonikuta huko; isipokuwa
Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki
vyaningoja,” Mdo 20:22-23
Mtume Paulo anajua wazi
maamuzi yake aliyoyachukua katika maisha msingi wake ni Kristo mwenyewe, na hajuutii
uamuzi wake huo. Siri yake ni kwamba, tunapojitoa kwake Kristo bila kujibakiza
tunauhakika wa uzima wa milele, na safari yetu kuelekea katika utumilifu huo wa
maisha ya umilele ni safari salama na yauhakika. Hivyo, “siyahesabu
maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma
ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu,”
Mdo 20:24.
Wapendwa wana wa Mungu,
tufanyapo maamuzi haya katika maisha licha ya magumu tunayokumbana nayo,
tunajua mbele yetu yupo Jemedari Mkuu Yesu Kristo aliyeyashinda yote, na
asiyeshindwa kwa lolote. Mateso na magumu tunayokutakana nayo katika maisha
Kristo anayajua, na ndiye yeye atakayetutoa kwenye mikwamo hiyo kiimani endapo
tutaweka matumaini yetu yote kwake kama mweza wa vyote. Katika ukweli huu Yesu
anasema, “Mimi nawaombea hao; siuombei
ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio
wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao,” Yoh 17:9-10. Je, kwa nini Yesu
hauombei ulimwengu? Ulimwengu huu ni kama tanuru la kufulia chuma. Kupata chuma
bora na imara lazima kipite kwenye moto mkali sana. Nasi katika kuyashinda
mateso haya hapa duniani ndivyo tunavyojiimarisha katika imani na kunyakua taji
ile tuliyoandaliwa. Kwa hiyo ulimwengu kama ulivyo ni sehemu ya kukomaza Imani
yetu na kukua Kiroho na kimwili.
Ndugu yangu, Je, mateso
na maisha yako kwa ujumla yana mwelekeo huo wa uzima wa milele yaani kumjua
Mungu wa kweli na Yesu Kristo?
Tumsifu Yesu Kristo!
EE MUNGU
NIWEZESHE MAISHA YANGU YA LENGE KUKUJUA WEWE MUNGU WA KWELI NA YESU KRISTO
MWANAO.
No hay comentarios:
Publicar un comentario