jueves, 5 de septiembre de 2019

TAFAKARI: IJUMAA YA WIKI YA 22 YA MWAKA-I


IJUMAA WIKI YA 22 YA MWAKA-I
Somo: Kol 1:15-20
Zab: 100: 1b-2, 3, 4,5
1      Dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba.
(K) Njoni mbele zake Bwana kwa kuimba.
2      Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)
3      Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake. (K)
4      Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)
Injili: Lk 5:33-39
Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,” Kol 1:16.
Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?” Lk 5:34.
“Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya,” Lk 5:38.
“Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema,” Lk 5:39.
TAFAKARI: “Nguvu na mamlaka ya Kristo ni uthibitisho wa ujemedari wake dhidi ya uovu.”
Wapendwa wana wa Mungu, mamlaka aliyokuwa nayo Yesu ni vita na ushindi dhidi ya uovu hapa duniani. Ni ukweli usiopingika kwa kupitia jina lake tunapata uponyaji wa kweli, Mdo 4:12. “Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende,” Mdo 3:6. “Mamlaka ya Yesu yamejengwa chini ya mamlaka ya Mungu. Hivyo hakuna jambo lolote alifanyalo Yesu Lisilo kuwa na uhusiano na Mungu, huku jambo lile likifunua siri ya Mungu kila kukichwa. “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,” Kol 1:16. Kwa nini basi nakuwa na mashaka juu ya utendaji wa Kristo katika maisha yangu?
Wapendwa katika Kristo, Yesu anapotoa mfano wa vazi kuukuu na jipya, na kwa upande mwingine divai ya zamani na kiriba cha kipya anataka kutufundisha jambo hili; kwanza kabisa lazima tujue sababu na malengo ya maisha yetu hapa tuniani. Hatupo hapa duniani kwa bahati mbaya hata kidogo. Tupo katika ulimwengu huu kadiri ya mpango wa Mungu ambao ni dhahiri na mathubuti. Hivyo lolote lile lililo jema mbele ya Mungu huwiishwa na kufanya upya. Katika Injili ya leo tunaona watu wakimletea Yesu malalamiko juu ya kufunga na kuomba. Kufunga kwetu na kuomba kwetu uifaidia kwanza kabisa roho zetu na wenzetu. Tunawajibu huo kiimani, na yatupasa kuutekeleza pasipo imani na msaada wowote. Ndiyo maana Yesu anawauliza watesi wake swali hili: “Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?” Lk 5:34. Maisha yapaswa kusherehekewa kwa sababu ni mali na zawadi ya Mungu.
Hivyo basi, upya wetu kiimani hutoshelezwa na upya tuupokeao kwa Yesu tunaposhiriki sakramenti zake tukiwa katika hali ya usafi. Hivyo “divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya,” Lk 5:38. Ndani na katika Kristo kiimani hujengeka kwa matendo madogo madogo yanayompendeza Mungu. “Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema,” Lk 5:39. Ndugu yangu ukiona vinaelea ujue vimeundwa.
Tumsifu Yesu Kristo!
“Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya,” Lk 5:38.
Tusali:-Ee Yesu Mwema, tuimarishe katika imani, na tuishi katika kweli yako. Amina

No hay comentarios:

Publicar un comentario